Kundi la wanamgambo wa Isalmic State siku ya jumapili lilikiri kutekeleza shambulio la kujitoa muhanga lililoua wanajeshi saba wa Jordan katika mpaka wa Syria.Taarifa hiyo ilitolewa kwenye tovuti ya shirika la habari la Amaq.
likinukuu chanzo ambacho hakikutajwa kwa jina, lilisema kuwa shambulio la jumanne dhidi ya kambi ya Jordan na Marekani mjini Rokban nchini Jordan lilitekelezwa na mpiganaji wa Islamic State.
Mlipuko, ambao pia uliwajeruhi wanajeshi 13 ulitokea katika eneo ambalo maelfu ya raia wa Syria wamepiga kambi.
Post a Comment