0
Urusi ilikuwa na mpango mahsusi wa kisiri wa kutoa madawa ya kuongeza nguvu mwilini kwa wanariadha wake walioshiriki mashindano ya msimu wa baridi ya Sochi.
Ripoti huru kuhusu madai ya matumizi ya madawa imebaini.
''Wizara ya michezo ya Urusi iliendesha ikadhibiti na kutekeleza mpango huo ikiwemo kubadilisha mikojo ya wanariadha iliyokuwa ikifanyiwa uchunguzi ''Ripoti hiyo inaeleza.
Kimsingi ripoti hiyo imethibitisha madai ya mkuu wa zamani wa mahabara inayoshughulikia madawa ya kuongeza nguvu za mwilini kuwa udanganyifu ilifanyika kwa kiwangio kikubwa na uliungwa mkono na serikali ya Urusi.
Bwana Grigory Rodchenkov alidai kuwa aliwapa chembechembe za madawa yaliyopigwa marufuku wanariadha kadhaa wa Urusi.
Image copyrightPA
Image captionUchunguzi huo huru uliendeshwa na Daktari Richard McLaren, kutoka Canada.
Uchunguzi huo huru uliendeshwa na Daktari Richard McLaren, kutoka Canada.
Uchunguzi huo umebaini kuwa alibaini mbinu ya kufungua chupa za kubeba mkojo na kubadilisha mikojo.
McLaren alituma chupa kadhaa za mkojo mjini London kubaini iwapo ilifunguliwa.
Image copyrightGETTY
Image captionUchungzi huo utaipa shinikizo kamati ya kimataifa ya olimpiki kukipiga marufuku kikosi chote cha Urusi kutoka kwa mashindano ya olimpiki
Uchunguzi wake ulibaini kuwa asilimia 100% ya chupa hizo za mikojo zilikuwa na dalili za kufunguliwa kabla na baada ya michezo ya msimu wa baridi ya Sochi mwaka wa 2014.
Uchungzi huo utaipa shinikizo kamati ya kimataifa ya olimpiki kukipiga marufuku kikosi chote cha Urusi kutoka kwa mashindano ya olimpiki ya mjini Rio ambayo yatafanyika china ya majuma matatu yanayokuja.
Michezo hiyo ya Olimpiki itaanza mjini Rio de Janeiro Brazil tarehe 5 Agosti.

Post a Comment

 
Top