0
Kasisi maarufu zaidi wa kishia nchini Bahrain amepokonywa uraia wake.
Mamlaka inasema kuwa Sheikh Qassim, amekuwa akieneza ujumbe wa utengano.
Taarifa hiyo pia inasema kuwa amekuwa akitumiwa na mataifa ya kigeni.
Haya yanajiri baada ya miaka mingi ya wasiwasi baina ya washia ambao ndio wengi nchini Bahrain, na serikali ya tiafa hilo ambayo inatawaliwa na wasunni.
Washia wanasema wamekuwa wakibaguliwa na wamekuwa wakidai marekebisho.

Post a Comment

 
Top