Israel na Uturuki wanatarajiwa leo kutia sahihi mapatano yanayonuia kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili.
Uhusiano wa karibu baina ya mataifa hayo uliharibika miaka sita iliyopita wakati wanamaji wa Israeli waliposhambulia meli ya Wanaharakati wa Uturuki waliokuwa wakipeleka msaada wa vyakula na madawa huko Palestina kwenye ukingo wa Gaza na kuwaua 10 kati yao.
Maafisa kutoka mataifa hayo mawili wanasema kuwa mapatano yameafikiwa kumaliza uhasama huo.
Uhusiano umeimarika tangu Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip kuwasiliana kwa simu mwaka wa 2013, kabla ya mashauriano kuanza na yameimarika kwa miezi michache iliyopita.
Miongoni mwa hatua za kwanza itakuwa kuwarudisha mabalozi wa mataifa hayo waliorejeshwa nyumbani baada ya meli ya wakereketwa wa Uturuki waliokuwa wakisafirisha chakula kuwapelekea Wapalestina kushambuliwa na Israel.
Aidha baadhi ya mapendekezo ni Israeli kuomba msamaha kwa uturuki na kisha kufidia wanaharakati waliouawa.
Post a Comment