0
Amri ya dini inayohalalisha ndoa za watu wanaobadili jinsia imeungwa mkono nchini Pakistan ,lakini wanaharakati wanasema tabia lazima zibadilike.
Amri hiyo au 'fatwa' ilipitishwa siku ya Jumapili na kundi la viongozi wa kidini.
Inasema kuwa watu waliobadili jinsia ambao wana ishara za kuonekana za kuwa wanaume ama wanawake wanaweza kuoa mtu wa jinsia tofauti.
Lakini wale wenye ishara zinazoonyesha jinsia zao hawawezi kuoa,imesema.
Viongozi hao wapatao 50 ambao ni miongoni mwa kundi linalojiita Tanzeem Ittehad-i-Ummat lenye makao yake huko Lahore pia limesema kuwa kitendo chochote cha cha kuwaudhi,kuwashambulia watu waliobadili jinsia kinafaa kuchukuliwa kuwa uhalifu chini ya dini ya kiislamu.

Post a Comment

 
Top