Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa limeingilia kati katika kukabiliana na virusi vya Zika huku kukiwa na wito kwa mashindano ya michezo ya Olimpiki kuahirishwa kufuatia mlipuko wa virusi hivyo.
Afisa wa WHO Bruce Aylward ameiambia BBC kwamba hatua za kukabiliana na ugonjwa huo zimekamilishwa.
Alikiri kwamba shirika la afya duniani WHO linaweza kufanya kazi nzuri zaidi kupitia kutoa tangazo kuhusu kile kinachoendelea na kwamba hakuna haja ya kuahirisha michezo hiyo.
Katika barua ya wazi wanasayansi 152 walisema kuwa utafiti waliofanya kuhusu Zika umeonyesha kuwa ni hatari kwa michezo hiyo kuendelea.
Pia wamesema kuwa shirika hilo la afya duniani linafaa kufuata maelezo yake kuhusu Zika.
Ugonjwa huo unahusishwa na watoto walio na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.
Kati ya Februari na Aprili,Brazil ilisajili zaidi ya visa 90,000 vya Zika.
Visa vya watoto waliohusishwa na virusi hivyo ni 4,908 kufikia mwezi Aprili
Post a Comment