0
Maelfu ya Waislamu wanahudhuria ufunguzi rasmi, wa msikiti wa kihistoria katika eneo la Bosnia linalotawaliwa na Serbia miaka 20 kamili, baada ya kuangamizwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Polisi wengi walikuwa zamu huko Banja Luka, wakati mabasi yaliyoleta Waislamu kutoka Bosnia, yaliwasili katika eneo hilo la msikiti Ferhat-Pasha, uliojengwa karne ya 16 hapo Banja Luka.
Mwandishi wa BBC anasema wakuu katika jimbo la Republika Srpska, wanataka kuondosha sifa yao ya WaSerb wenye msimamo mkali wa kizalendo, na kutaka waonekane kuwa wanakaribisha tamaduni tofauti.
Tarehe 7 sasa inaadhimishwa kuwa siku ya msikiti nchini Bosnia, ambako misikiti 614 iliangamizwa katika vita vya mwaka 1992 hadi 1995

Post a Comment

 
Top