Dawa ya maumivu Ibuprofen na dawa ya kutibu saratani Toremifene zinaweza kukata makali ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ,watafiti wamesema.
Wanasayansi walitumia Kifaa cha Diamond Light Source kuvifanya uchanganuzi virusi vya ebola kwa kina.
Walibaini kwamba dawa hizo mbili zinaweza kushirikiana kukabiliana na Ebola wakati virusi hivyo vinapojiandaa kuambukiza seli za mwili wa bindamu.
Hatahivyo ,watafiti hao wameonya kwamba huo ni mwanzo na kwamba dawa zaidi zilizo na uwezo mkubwa zinafaa kutafutwa.
Synchrotron hiyo huchochea kasi ya elektroni hadi kuzalisha mwanga mkali sana.
Hii inaweza kutumika kwa kuchambua mradi wa kutengeza vitu wa atomiki katika mpango mkubwa zaidi kuliko darubini za kawaida.
Lengo la utafiti huo ni protini kwenye uso wa virusi vya Ebola ambayo inaviruhusu kuambukiza seli.
''Hili ndio lengo kuu katika uso wa virusi hivyo,hili ndio huwajibika kujiweka katika seli ,ni protini muhimu kuelewa'',alisema mtafiti Prof Dave Stuart, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.
Post a Comment