Mwanakandanda mlinzi wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Paris St-Germain, Serge Aurier atafikishwa mahakamani mnamo Septemba tarehe 26 kwa kumpiga askari polisi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa na polisi Jumatatu kwa kosa la kumshika mashati afisa wa polisi na kukaidi amri nje ya klabu kimoja cha usiku mjini Paris.
Aurier kwa upande wake amewasilisha kesi mahakamani dhidi ya maafisa wa polisi waliomkamata akidai kuwa walimnyanyasa na kumpiga.
Makabiliano hayo yamkini yalitokea katika eneo la burdani la Champs Elysees Aurier alipokuwa akitoka klabuni.
Maafisa wakuu wa klabu yake ya Paris St Germain wanasubiri mawasiliano rasmi kabla ya kutangaza hatua watakayochukua.
Kocha Laurent Blanc alimsimamisha kazi kwa muda Aurier mwezi Februari mwaka huu kwa tuhuma za kuchapisha video kwenye mtandao wake wa kijamii akiwakashifu kocha huyo na wachezaji wenza wa PSG, Zlatan Ibrahimovic na Angel di Maria.
Post a Comment