0
20:45 Bolasie naye anashambulia upande ule mwingine. Lakini hafanikiwi.
20:44 Fellaini anapata mpira mzuri eneo la hatari kutoka kwa Rashford, lakini linazuiwa.
20:40 Scott Dann ndiye mchezaji wa kwanza wa Palace kuadhibiwa. Anapewa kadi ya njano kwa kumwangusha Marcus Rashford.
20:37 Kipindi cha pili kinaanza.
  • Manchester United 0-0 Crystal Palace
20:21 Ni wakati wa mapumziko.
20:19 Juan Mata wa United anaoneshwa kadi ya njano kwa kumchezea visivyo Pape Souare.
20:15 Crystal Palace wanashambulia tena lakini refa Mark Clattenburg anarejesha mchezo nyuma. Joel Ward alifanyiwa madhambi na Marcos Rojo analishwa kadi ya njano.
20:10 Wilfried Zaha anapata mpira na kukimbia nao lakini anakabiliwa na Wayne Rooney, anaanguka.
Image copyrightPA
20:08 Anthony Martial anapata krosi safi kutoka kwa Marcus Rashford eneo la hatari, lakini kombora lake linazimwa na Joel Ward .
20:02 Yannick Bolasie anapata fursa na kutoa kombora kali. De Gea anaokoa.
19:59 United wanapata kona. Fellaini anakaribia kufunga kwa kichwa, lakini mpiga unatolewa nje. Inakuwa kona nyingine lakini haizai matunda.
19:57 Mata anatoa kombora kali. Linatulizwa kidogo na kipa Hennessey lakini mpira bado unasonga. Mchezaji wa Palace anaufagia na kuuondoa hatarini.
19:53 Mpira wa adhabu unapigwa na Yohan Cabaye na Yannick Bolasie anaugusa kwa kichwa na karibu utue wavuni lakini De Gea anautupa juu ya wavu.
19:52 Mchezaji wa Palace Wickham anakabiliwa na Smalling, anaangushwa lakini anajinyanyua na kufunga. Lakini bao linakataliwa. Mwamuzi anarejesha mpira nyuma na unakuwa mpira wa adhabu. Smalling anapewa kadi ya njano.
19:51 Rooney kutoka nje ya eneo la hatari anatoa krosi safi kwa Marcus Rojo ambaye anatoa kombora. Lakini kipa wa Palace Hennessey anaudaka.
19:49 Rooney anatoa kombora ambalo kidogo linamzidi kipa wa Palace anayeutema lakini baadaye anafanikiwa kuufikia.
19:48 David de Gea analazimika kutumia ujanja kuzuia mpira kutoka nje.
19:45 Rashford anapata mpira eneo la hatari, anatoa kombora lakini linazuiwa na inakuwa kona. Fellaini anajaribu kuufikia mpira kwa kichwa bila mafanikio.
Image copyrightREUTERS
19:43 United wanapata kona nyingine, hii inapigwa juu lakini haizai goli.
19:41 Rashford anajikakamua kupitia winga na kujaribu kuelekea kwenye lango la Palace. Anakabiliwa Damien Delaney na kutoa mpira nje. Lakini Palace wanazawadiwa kona ambayo inapigwa fupi.
19:40 United wanapata kona. Inapigwa kona fupi. Lakini haizai matunda.
19:39 Palace wanapata kona. Lakini mpira unatua mikononi mwa De Gea.
Image copyrightEPA
19:38 Klabu zote mbili zinashambulia.
19:35 Mechi inaanza.
19:30 Mwanamfalme William anawasalimia wachezaji wote 22.
19:29 Wachezaji wanaingia uwanjani.
18:59 Wachezaji kwa sasa wanapasha misuli moto. Mechi itaanza saa moja unusu. Kuna dakika 30 hivi kabla ya kipenga cha kwanza kupulizwa.
18:33 Wachezaji watakaoanza mechi leo wametangazwa.
Image copyrightGETTY
Manchester United wamefanya mabadiliko mawili, Marouane Fellaini amerejea kikosini.
Kikosi cha Man Utd: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Fellaini, Mata, Rooney, Martial, Rashford
Image copyrightALL SPORT
Crystal Palace: Wilfried Zaha anaanza mechi hii ya Wembley.
Kikosi cha Palace: Hennessey; Ward, Dann, Delaney, Souare; Zaha, Cabaye, McArthur, Jedinak, Bolasie; Wickham.
18:31 Mechi ya leo ni kama marudio ya fainali ya 1990. Mechi ya kwanza timu hizo zlitoka sare 3-3 lakini mechi ya marudiano, Manchester United wataondoka na kikombe baada ya kushinda 1-0.
18:30 (Saa za Afrika Mashariki): Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya Fainali ya Kombe la FA.


Manchester United wanashuka dimbani dhidi ya Crystal Palace uwanjani Wembley.

Post a Comment

 
Top