Mahakama ya Misri, imeahirisha kesi ya rais wa zamani, Mohamed Morsi, na watu wengine 10, kwa mashtaka ya kutoa siri za taifa kwa Qatar.
Kesi za washtakiwa sita pamoja na waandishi wa habari wane, zitapelekwa mbele ya Mufti mkuu, hatua inayoonyesha kwamba wamehukumiwa kifo.
Mufti ataamua kama hukumu hizo zitekelezwe.Bwana Morsi hayumo kati ya washtakiwa hao 6.
Amekabiliwa na kesi kadha tangu jeshi, lilipomtoa madarakani mwaka wa 2013 na amewahi kuhukumiwa kifo.
Post a Comment