Wakuu wa jeshi la wanamaji la Uchina, wanasema wanawasaka watu 17, waliotoweka, baada ya mashua kugongwa na kuzamishwa na chombo cha nchi za nje, katika bahari ya mashariki ya Uchina.
Watu wawili kati ya 19 waliokuwemo ndani ya mashua hiyo, waliokolewa wakiwa hai.
Wakuu wanasema kazi ya kuwasaka watu hao ni ngumu, kwa sababu ya wingu, nje ya mwambao wa jimbo la Zhejiang.
Wakuu hawakusema chombo kilichogonga mashua yao ni cha nchi gani
Post a Comment