0
Idara ya sheria nchini Marekani inataka kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mtu aliyewaua kwa kuwapiga risasi watu katika kanisa mjini Charleston ambapo watu 9 waliuawa.
Mkuu wa sheria Loretta Lynch, alisema kuwa kiwango cha uhalifu huo kinatosheleza kutolewa kwa hukumu ya kifo
Dylann Roof anashtakiwa kwa mauaji ya waumini tisa katika kanisa moja la watu weusi , jimbo la South Carolina.
Image copyright
Image captionPolisi wanasema kuwa Roof alikaa na waumini kwa muda wa saa moja kabla ya kuanaa kuwafyatulia risasi.
Polisi wanasema kuwa Roof alikaa na waumini kwa muda wa saa moja kabla ya kuanaa kuwafyatulia risasi.
Mwanamme huyo wa umri wa miaka 22, alikuwa akihudhurua mafunzo ya Biblia katika kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal mwezi Juni mwaka uliopita wakati aliwashambulia waumini.
Anakabiliwa na mashtaka 33 yakiwemo yanayohusu chuki, kuzuia dini na mengine yanayohusu silaha.
Polisi wanasema kuwa aliwalenga watu kutokaka na rangi yao

Post a Comment

 
Top