Timu ya taifa ya soka ya Kenya harambee stars imeanza kambi rasmi ya mazoezi mjini Nairobi zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kucheza dhidi ya Tanzania katika mechi ya kirafiki.
Wachezaji wa timu hiyo maarufu kama Harambee Stars wakiongozwa na kocha Stanley Okumbi walikusanyika uwanjani Kasarani na kufanya mazoezi ya kwanza Jumanne asubuhi.
Miongoni mwa wachezaji waliofika kambini ni wachezaji wanaosakata soka ya kulipwa katika ligi za nje ya Kenya.
Wachezaji wa timu ya Zesco ya Zambia wakiwemo Jesse Werre, David Owino na Anthony Akumu walikuwa baadhi ya wachezaji waliowasili.
Kiungo wa Southampton Victor Wanyama hakuwa amewasili na anatarajiwa kujiunga na timu hiyo wiki hii.
Baadhi ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi walipewa ruhusa kuziwasilisha timu zao za ligi kwa minajili ya mechi za ligi zinazochezwa wiki hii.
Kenya itaachuana na Tanzania tarehe 29 mjini Nairobi siku chache kabla ya kuialika Congo kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la Afcon 2017.
Wakati huo huo, timu ya wachezaji chipukizi wa Kenya wanatarajiwa kucheza dhidi ya Sudan Tarehe 27.
"Tunalenga kucheza mechi za kirafiki za kutosha ikiwezekana, ingawa sio kazi rahisi,’’ rais wa shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa alisema.
Kenya imo katika kundi E ikiwa na alama moja baada ya kucheza mechi nne
Post a Comment