0
Simba zaidi ya 30 ambao wameokolewa kutoka kwa makundi ya wanasarakasi Peru na Colombia watahamishwa na kupelekwa Afrika Kusini.
Wanyama hao waliokuwa wanatumiwa na wachezaji wazungukao mjini kuonyesha michezo yao waliteswa na kudhalilishwa, kwa mujibu wa kundi la kutetea haki za wanyama la Animal Defenders.
Image copyrightAP
Simba mmoja alipofuka.
Wengine wengi walikatwa kucha zao.
Image copyrightAP
Kundi hilo la Animal Defendersndilo lililopanga shughuli hiyo ya kuwasafirisha wanyama hao.
Ndiyo shughuli kubwa zaidi kuwahi kuandaliwa ya kuwasafirisha simba.
Image copyrightAP
Simba hao watafungiwa kwenye vizimba kama hivi na kusafirishwa Ijumaa.

Post a Comment

 
Top