Chama cha upinzani nchini Tanzania
Chadema kimeuliza maswali mengi kuhusu hatua zilizopigwa katika
uchunguzi wa Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu ambaye mwezi
uliopita alipigwa risasi mjini Dodoma na sasa amelazwa katika hospitali
ya Nairobi kwa matibabu.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya
habari , Mkurugenzi mshirikishi na usajili wa chama hicho Benson
Kigailia amesema kuwa kufikia sasa hakuna mtu aliyetiwa mbaroni ili
kusaidia katika uchaguzi huo.Kulinaga na gazet la The Citizen Tanzania ,alisema kwamba katika eneo la Kibiti, ambapo mashambulizi na mauaji yamefanyika hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuhakikisha kuwa washukiwa wanakamatwa.
Akielezea zaidi , alisema kuwa ni rahisi kwa maafisa wa usalama kuchunguza , kuwatafuta na kuwakamata watu wanaomkosoa rais katika mitandao ya kijamii badala ya kuchunguza na kuwakamata washukiwa wanaotaka kuwaua wengine mchana kutwa.
Gazeti hilo limenukuu akisema kuwa mbali na kuyakamata magari 10 kuhusiana na jaribio hilo la mauaji, la kushangaza ni kwamba hakuna hata mlinzi mmoja aliykuwa kazini katika eneo la Area D mjini Dodoma amekamatwa'', alisema.
Post a Comment