Bayern Munich imemuajiri aliyekuwa
kocha wake wa zamani Jupp Heynckes kama mkufunzi wao mpya hadi mwisho wa
msimu huu kufuatia kufutwa kazi kwa Carlo Ancelotti.
Ancelotti
aliondoka mwezi Septemba huku miamba hiyo ya Ujerumani ikiwa katika
nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya viongozi wa ligi Borussia Dortmund kwa
alama tano.Heynckes mwenye umri wa miaka 72 ameifunza Bayern mara tatu mwisho ikiwa 2013 wakati ambapo timu hiyo ilishinda kombe la vilabu bingwa, Bundelsiga na Kombe la Ujerumani kwa mara tatu.
''Ningependa kurudi katika klabu yoyote ilie duniani'', alisema.''Bayern Munich iko karibu na moyo wangu'' .
''Mimi na wafanyikazi wangu tutatumia kila njia ili kuleta tena ufanisi wa soka kwa mashabiki.Niko tayari kukabiliana na changamoto hiyo''.
Post a Comment