0
Timothy Weah, mwana wa mchezaji bora wa soka wa mwaka 1995 George Weah , alifunga bao la ushindi huku Marekani ikiishinda Cuba 6-2 mjini Panama na hivyobasi kufuzu kwa kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 17.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 kutoka Rosedale, New York ambaye yuko katika timu ya kinda wa PSG , alimsaidia Zyen Jones katika dakika ya 49 na kuiweka kifua mbele Marekani kwa 4-2 kabla ya kufunga bao lake la pili katika mashindano hayo ya kaskazini, Marekani ya kati na eneo la Carribean katika dakika ya 88.
Bryan Renolds alipata bao la tano katika dakika ya 83 baada ya mkwaju wa Weah kupanguliwa na Echeverria kabla ya kuanguka katika miguu ya Reynolds.
Marekani sasa itacheza dhidi ya Mexico ama Costa Rica siku ya Jumapili katika fainali za CONCACAF.

Post a Comment

 
Top