Kimbunga Irma kimepiga jimbo la Florida nchini Marekamani
Irma kwanza kabisa kilipiga kisiwa cha Marco magharibi mwa pwani mwa Florida, kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 192 kwa saa lakini tangu kwa sasa kimeshuka kutoka kiwango cha tatu hadi cha pili.
Zaidi ya nyumba milioni 3.4 katika jimbo la Florida hazina nguvu za umeme na sehemu za mji wa Miami zimefurika maji.
Vifo vitatu vinavyotokana na kimbunga hicho vimeripotiwa wakati Irma kikielekea sehemu za kaskazini.
Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema Irma kimesababisha upepo sehemu tofauti za katikati mwa Florida.
Mapema kimbunga hicho kilipiga maeneo yanayozunguka mji wa Fort Myers.
Irma tayari kimeharibu sehemu za Caribbean na kuya takriban watu 28.
Watu milioni 6.3 huko Florida wameambiwa wahame.
Post a Comment