Nyota wa Barcelona Neymar amepewa
ruhusa ya kuondoka Barcelona akitarajiwa kujiunga na PSG katika kitita
cha rekodi ya pauni milioni 198.
Raia huyo wa Brazil amewaambia wachezaji wenzake wakati wa mazoezi siku ya Jumatano kwamba angependa kuondoka.- Kwa nini Neymar anataka kuondoka Barcelona?
- PSG wamtafuta Neymar
- Neymar kufikishwa kizimbani
- Mahakama yataka Neymar kufungwa miaka 2 jela
Mshambuliaji huyo ataruhusiwa kuondoka kwa gharama ya Yuro milioni 222, ambazo PSG iko tayari kulipa.
Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya kubainika kwamba Barca ilikuwa tayari kuruhusu uchunguzi wa Fifa iwapo PSG ingemsajili Neymar.
Katika mahojiano na gazeti la Mundo Deportivo, rais wa La Liga Javier Tebas alitishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Ligue 1 iwapo soka ya Ulaya itashindwa kuchukua hatua.
Pia alisema kuwa rais wa PSG Nasser Al Khelafi alijulishwa kuhusu malengo ya mabingwa hao wa Uhispania.
Neymar alihamia Barcelona kutoka klabu ya Santos nchini Brazil 2013 kwa uhamisho wa pauni £46.6m na kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Uhispania 2016.
Mwakilishi wake Wagner Ribeiro ambaye siku ya Jumatano alichapisha ujumbe wa Twitter akisema yuko mjini Paris alisema mwaka uliopita kwamba mteja wake atalipwa mshahara wa £650,000 kwa wiki bila kutozwa kodi iwapo atajiunga na klabu hiyo ya Ufaransa.
Uvumi kuhusu uhamisho huo wa Neymar ulizuka , lakini rais wa klabu hiyo Jospe Maria Bartomeu aliambia BBC mchezaji huyo atasalia.
Neymar aliichezea klabu hiyo ya Barcelona katika mashindano ya ubingwa nchini Marekani kabla ya kusafiri kuelekea China ili kutimiza maswala yake ya kibishara.
Alisafiri kuelekea Uhispania siku ya Jumanne kabla ya kurudi Barcelona siku ya Jumatano.
Mchezaji huyo wa Barcelona aliifungia Barcelona mabao 105, kuisaidia kushinda mataji 2 ya ligi ,mataji 3 ya Copas del Rey na moja la vilabu bingwa Ulaya.
Post a Comment