Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi
inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana
wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiadhibiwa kufuatia
majaribio ya makombora.Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili.
Akizungumza katika baraza hilo wawakilishi David Ciciline kutoka chama Democratic amesema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.
Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.
Naye Ted Poe kutoka chama cha Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia.
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la Urusi Duma , Leonid Slutsky amesema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani
Post a Comment