Mjumbe mpya wa Marekani nchini
Ukrian anasema kuwa Marekani inatathmini ikiwa itatuma silaha kusaidia
wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na Urusi.
Kurt Volker aliiambia BBC kuwa kuihami serikali ya Ukrain itabadilisha msimamo wa Urusi.Alisema hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi.
- Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandao
- Mapigano mapya mashariki mwa Ukrain
- Ukrain yakiuka onyo la Urusi na kufanya mazoezi ya kijeshi
"Silaha za kujilinda, zile ambazo zitaisaidia ukrain kujilinda na kuharibu vifaru kwa mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukrain," bwana Volker aliiambia BBC.
Alisema kuwa mafanikio ya kuwepo amani mashariki mwa Ukrain yanahitaji kile alichokitaja mchakato wa mazungumzo na Urusi.
Bwana Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye Nato na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu.
- Trump aitaka Urusi kuwacha kuivuruga Ukrain
- Urusi kuvuruga matangazo ya radio kutoka Ukrain kwenda Crimea
Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao
Post a Comment