Golikipa wa zamani
wa timu ya taifa ya Nigeria Vincenti Enyama, ni moja kati ya wachezaji
kumi na moja walioambiwa na kocha wa Lille,Marcelo Bielsa, hawahitajiki
katika klabu hiyo msimu ujao.
Enyama ambae aliichezea timu ya
taifa ya Nigeria michezo 101 alisaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu
hiyo kwa muda mrefu msimu uliopitaBielsa ambae ni kocha mpya katika timu hiyo pia amewatumia ujumbe mchezaji Stoppila Sunzu,raia wa Zambia, Mtunisia Naim Sliti na Junior Tallo kutoka Ivory Coast kuwataarifu hawako katika mipango yakeLille tayari imemsajili golikipa wa kimataifa wa Burkina Herve Koffi, mabadiliko haya yanakuja baada ya timu hiyo kumaliza katika anfasi ya kumi na moja msimu uliopita.
Post a Comment