0
        PHONE NO:+255624031936 or +255768550136                                                                  
    TOVUTI:sitnewztanzaniablogspot.com                                                                             
                                                                                                                                                                                                                                                                    Na mwandishi wetu Magdalena marko       




                                                     Hili ndiyo tunda aina ya papai

Mpenzi msomaji wa makala ya AFYA YA JAMII ni wasaa mwingine wakufahamu mambo mbalimbali kuhusu matunda ikiwa leo tutaangalia  nini maana ya tunda aina ya Papai, tunda hili linalimwa zaidi katika ukanda gani na nini faida zake .ungana nami mwazo hadi tamati mwa makala hii .
Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili.Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi.
           
Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadirio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la 32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne
 Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -

                                1:MBEGU ZA  KAWAIDA  (LOCAL SEEDS)
                                                                                                                                                                      
 Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume huachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.

                     2. MBEGU CHOTARA (HYBRID SEEDS)

Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji

Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana unaweza kujirutubisha wenyewe

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo refu zaidi au umbo la pear.

Katika suala zima la kufanikisha makala hii  kuonekana katika ukurasa huu wa BONGO ENTERTAIN nilifanikiwa kukutana na mkulima wa zao hili ambae ni Bi Fortunata Daniel nae alieleza  kuwa Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno ambapo  ni takribani muda wa miezi 8-9 mpaka pale yanapoonekana sokoni. 
               “tunda aina  ya  papai huchukua muda mfupi sana ikiwa ni  ndani ya miezi 8-9 mpaka kufikia hatua ya mavuno na tayari kwa kutumiwa(kuliwa) na binadamu”Alisema mkulima wa papai bi Fortunata Daniel

      Lahaulah!!......ekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-2500. Mavuno ya mapapai kwa miezi 8 - 9 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 - 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 8 - 9. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utakapokufa..


Mpenzi msomaji moja kwa moja AFYA YA JAMII ilifanikiwa kuchukua maoni mbalimbali kwa watumiaji au walaji wa tunda hili ya papai  na wamepata kueleza faida za kula papai ambapo Bi Beatrice Mushi alitoa maoni yake na kueleza kuwa papai ni tunda mojawapo linalomsaidia katika umeng’enyaji wa chakula pindi anapomaliza kula chakula na pia inamsaidia kulainisha choo  na pia ni dawa kutokana na mmatetere yake kutibu minyoo pamoja ugonjwa wa malaria  ” siyo lazima daktari akwambie utumie matunda tujifunze kula matunda ili kulinda afya zetu na magonjwa ‘’ alisema betriace mushi mlaji wa tunda aina ya papai

Aidha Godyfrey Naano hakusita kueleza kile anachojua kuhusu tunda la papai na kusema kuwa yeye ni mlaji mzuri wa papai na humsaidia mwili wake kutokushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama EBOLA na MALARIA kwani papai ni tiba tosha katika mwili wa binadamu

Kufuatia tafiti mbalimbali  Papai ni moja ya tunda mashuhuri linalotumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida  nyingi mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili.
Baadhi ya jamii zimekuwa zikichukulia kirahisi ulaji wa matunda,lakini yakupasa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu

Vilevile, mtaalam waAfya  Bi Joan Hilary nae  anaeleza kwamba, watu wenye matatizo ya kupatwa na majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai, hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.                                                                                                                                                                                                                                          
               “watu wanaotokwa na majipu,uvimbe na vidonda kila wakati wana wamepungukiwa na virutubisho muhimu  vinavyopatikana kwenye papai ”alisema  joan Hilary
Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema wakatumia tunda hili mara kwa mara ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara, ingawaje ni vyema wakakumbuka matumizi ya sigara si mazuri kwa afya hivyo ikibidi ni vizuri kuacha kabisa.
Ni wazi kuwa papai ni tunda lililosheheni kila aina ya utajiri wa vitamin kuliko matunda mengine, kwani lina vitamin A, B, C, D na E.

Wataalam wa tiba za asilia pia wanaeleza kwamba tunda hili linauwezo wa kutibu tatizo la usagaji wa chakula tumboni pia hutibu kisukari na pumu na mara nyingine hata kifua kikuu.
Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa:

Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
Kutibu Udhaifu wa tumbo
Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
Kutibu Kifua kikuu

Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho, kama inavyoaminika kwa karoti, hali kadhalika papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara


 Kutana nami katika mwendelezo wa makala kuhusu matunda mbalimbali ambapo hapo kesho tutaenda kuangazia tunda aina ya chungwa upate kujua mambo kadha wa kadha kuhusu tunda hilo pamoja na faida zake

Post a Comment

 
Top