0
Wakazi wa Mji wa Mogadishu nchini Somalia walalamikia gharama wanazotozwa ili kupata vitambulisho vilivyotolewa na Serikali.
Serikali inawatoza takriban dola 20 zikiwa ni gharama za kupata kadi ya kielektroniki ambapo Serikali imesema lengo ni kuimarisha usalama na kuwawezesha kuwatambua watu mjini humo.
Utoaji na upatikanaji wa vitambulisho vya kitaifa ni mojawapo ya huduma zilizotoweka tangu kuanguka kwa serikali ya utawa wa Siad Bare Zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Post a Comment

 
Top