0
Wanasayansi wamethibitisha kwamba aina ya kunguru mwitu kutoka New Caledonia kusini mwa Pacific wanaweza kutengeneza zana.
Ndege hao walichunguzwa walipokua wakitumia midomo yao kuchukora chakula kilichokua kimefichwa kati kati ya mbao.
Awali ujuzi huu ullibainika kwa ndege wanaotunza kwenye maabara .
matokeo ya uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Open Science, yanasema kuwa kipaji hiki ni sehemu ya tabia asilia ya ndege.
Mwaka 2002, kunguru mwitu anaetunzwa kwenye maabara ya New Caledonian crow - kwa jina Betty - aliwashangaza wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford walimpatia chakula katika kikapu kisichoweza kufikiwa kwa urahisi.
Kukifikia , ndege huyo alipindisha kipande cha waya hadi ndani ya kikapu. Ilikua ni mara ya kwanza kwa ujuzi huo wa kutengeneza kifaa kuwahi kushuhudiwa katika ulimwengu wa wanyama.
Betty alikufa mwaka 2005, lakini baada ya miaka, hatimae uchunguzi ulifanikiwa kurudiwa katika ndege mwingine alieko kwenye maabara.
Mkuu wa uchunguzi huo Dr Christian Rutz, kutoka chuo kikuu cha St Andrews cha Scotland, anasema : "ilionekana ni kama ni kitu ambacho ndege yule alikivumbua katika maabara ."
Wakati inafahamika kwa muda mrefu kwamba kunguru wa porini huweza kudonoa vitu kutoka kwenye sehemu zilizojificha za ndani , watafiti sasa wamebaini kuwa wanaweza pia kupindisha vijiti sawsa na wenzao wa maabara.
Kunguru mwituImage copyrightRUTZ GROUP
Image captionKunguru 10 kati ya 18 waliweza kutengeneza vijiti vya kudonolea chakula
Katika msururu wa uchunguzi , watafiti waliwakamata kunguru kutoka misitu ya New Caledonia, na kuwaweka kwa muda mfupi katika viota vya muda
Dr Rutz anasema: "Hii inamaanisha kwamba tunaweza kuwafanyia majaribio katika hali ya uchunguzi unaodhibitiwa zaidi - lakini aina za vipimo tunavyofanya pale, havionyeshi vema namna ndege hawa walivuyo na akili , wanauliza ni aina gani ya kifaa ambacho wanakielezea kwa tabia asilia.
Kunguru walipewa vijiti , ambavyo vilikua na ladha ya chakula ambavyo viliwekwa kwenye mashimo kwenye sakafu
"Kitu kimoja tu tulichowapatia ulikua ni mmea ambao tulifahamu kwa kawaida wanatumia kutengenezea kifaa mwituni ," alieleza Dr Rutz.
"kwa hiyo kazi ilikua rahisi sana , tuliomnba ndege wetu watengeneze vifaa kisha tuvitumie kutoa chakula kilichofichwa ."
Kunguru hawakuhitaji vijiti maridadi kuchukua chakula , lakini 10 kati ya 18 wa mwituni walifanya hivyo.

Post a Comment

 
Top