0
Makao makuu ya kijeshi ya Marekani, The Pentagon, yametangaza kuwa watu 15 waliokuwa wakizuiliwa katika gereza maalumu la Guantanamo Bay, nchini Cuba wamehamishiwa hadi Emarati.
Ni kundi kubwa zaidi kuwahi kuhamishwa kutoka gereza hilo chini ya utawala wa Rais Barack Obama.
Kumi na mbili kati yao wanatoka Yemen na watatu Afghanistan.
Wanachama wakuu wa chama cha Republican wamekosoa hatua hiyo.
Hatua hiyo inapunguza wafungwa hadi 61 wanaozuiliwa katika kituo hicho cha Marekani.
Mara kwa mara Bwana Obama ameeleza masikitiko yake juu ya msimamo wa wanachama wa Republican wa kupinga mpango wake wa kutaka kufunga gereza hilo.

Post a Comment

 
Top