0
TIMU ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jana ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya vijana wenzao wa Afrika Kusini katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo.
Habari kutoka Johannesburg ilipochezwa mechi hiyo zinasema mabao yote yalifungwa kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti.
Bao la Serengeti liliwekwa kimiani na Ali Mtengi katika dakika ya 30 na la Afrika Kusini lilifungwa na Luka de Roux dakika ya 45 Matokeo hayo yanaiweka Serengeti Boys katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwani inahitaji ushindi wa kuanzia bao moja katika mechi ya marudiano itakayochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi wiki mbili zijazo.
Serengeti ilifuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Bakari Shime inatarajiwa kurejea nchini leo tayari kwa mechi ya marudiano.
Michauno ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo itafanyika mwakani Madagascar.

Post a Comment

 
Top