0
Meneja wa timu ya taifa ya riadha ya Kenya katika olimpiki aliyetuhumiwa kuitisha hongo ya pauni (£10,000) amefikishwa mahakamani punde baada ya kurejeshwa mjini Nairobi.

Meja mstaafu Michael Rotich alirejeshwa nyumbani baada ya jarida moja nchini Uingereza la Sunday Times kuchapisha video iliyomuonesha akiitisha hongo ya pauni (£10,000) ilikuwadokezea wanariadha saa na siku watakapo wasili maafisa wa shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini WADA katika kambi ya mazoezi ya wanariadha nchini Kenya.

Rotich alifikishwa katika mahakama ya Milimani punde baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akitokea Rio de Jenairo.
Mahakama iliamua kuwa atasalia korokoroni katika kituo cha polisi cha Gigiri uchunguzi ukiendelea.
Kiongozi wa mashtaka ameiomba mahakama siku saba kukamilisha uchunguzi.
Katika muda huo uchunguzi utazuru kambi za mazoezi za wanariadha zilizoko Iten, Eldoret, Kapsabet na Kitale.
Gazeti hilo la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ARD zilimrekodi afisa huyo bila yeye kujua kuwa alikuwa akirekodiwa akiahidi kuwajulisha wanariadha siku ambayo maafisa wa kuchukua vipimo wa shirikisho la kupambana na madawa WADA watakapowasili Kenya.
Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini nchini Kenya ADAK Japhter Rugut aliahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.
Madai hayo yalitokea siku mbili tu baada ya shirika la kupambana na madawa duniani WADA kuiondoa Kenya kwenye orodha ya mataifa yanakiuka kanuni za vita dhidi ya udanganyifu michezoni na utumizi wa madawa ya kusisimua misuli.
Kwa mujibu wa mwandishi mpekuzi Hajo Seppelt, Meja Rotich amekuwa akishirikiana na watu wanaoendesha mpango huo wa siri wa kutoa dawa za kusisimua misuli kwa wanariadha.
Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.Image copyrightAFP
Image captionKenya yakabiliwa na madai mapya ya utumizi wa madawa
Meja huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha kenya kilichoshiriki katika guaride la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ijumaa iliyopita.
Takriban wanariadha 40 wa Kenya wamepatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika siku za hivi punde.

Post a Comment

 
Top