0
Katika hatuaambayo haikutarajiwa rais wa Urusi Vladimir Putin amemfuta kazi mkuu wake wa majeshi wa muda mrefu Sergei Ivanov.
Bwana Ivanov amekua miongoni mwa wandani wa Bw Putin anao waamini kwa miaka mingi.
Ivanov mwenye umri wa miaka 63 kwa sasa amekua pewa jukumu la kuwa mwakilishi katika masuala ya mazingira na uchukuzi.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kremlin imesema Bw Putin ana "mamlaka ya kumuondoa Ivanov kwenye majukumu yake ya kikazi kama rais wa Urusi ", lakini haikueleza ni kwa nini.
Naibu wa Ivanov tangu mwaka 2012, Anton Vaino, ndie aliyeteuliwa kurithi wadfa huo.
Bw Vaino mwenye umri wa miaka 44 ni mwanadiplomasia wa zamani.
Alizaliwa katika mji mkuu wa Estonian-Tallinn mwaka 1972, na alihitimu katika chuo kikuu cha kitaifa cha kifahari cha Moscow State Institute of International Relations (MGIMO) na kuhudumu kama balozi mjini Tokyo.
Baadae alimudu kuwa mkuu wa itifaki ya rais na wafanyakazi wa serikali, kwa mujibu wa ikulu ya Kremlin nchini Urusi.
Baada ya kuchaguliwa kwake, alimwambia Bw Putin: " Asante kuwa na imani nami. Nafikiri lengo kuu la utawala ni kuunga mkono shughuli zako kama kiongozi wa taifa katika kuandaa sheria na kuhakikisha maagizo yako yanatekelezwa."
Bw Ivanov alichukua wadfa wa mkuu wa majeshi mwezi Disemba 2011. Aliwahi kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi.

Post a Comment

 
Top