0
Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia nchini Zimbabwe wametumia gesi ya kutoa machozi na maji, kutawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu Harare.
Waandamanaji hao, waliokuwa na nia ya kuelekea hadi kwenye makao ya bunge kutoka upande wao walirusha mawe
Wanafunzi waliohitimu lakini wakakosa kazi pia walijiunga na maandamanoImage copyrightAP
Image captionWaandamanaji walibeba mabamngo ya kumtaka Mugabe ajiuzulu
Waliandamana huku wakipeperusha mabango yenye maandishi "Rais Mugabe lazima ang'atuke" na "umefeli bwana Mugabe"
Wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa miongoni mwa waandamanaji, na wanasema maandamano hayo hayakuchochea vurugu.
Waandamanaji walijitokeza kumtaka Mugabe ajiuzuluImage copyrightAP
Image captionPolisi watumia nguvu kuvunja maandamano
Baadhi ya waandamanaji wanapinga mpango wa serikali kuanzisha noti nyenginezo aina ya zile zinazoitwa 'bond notes' ambayo inasemekana italingana na thamani ya dolla ya Marekani.
Uchumi wa Zimbabwe umekumbwa na mdororo wa mda mrefu kiasi cha sarafu ya nchi hiyo kukosa thamani pakubwa.
Walimtaka Mugabe ajiuzulu kwa 'kuiangusha' ZimbabweImage copyrightAP
Image captionPolisi walitumia nguvu kuwatawanya waandamanaji
Mwezi jana chama cha ma- veteran wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe ambacho kimekuwa kikimuunga mkono kwa dhati rais Mugabe, kilikumbwa na mgawanyiko huku wengine wakikashifu vikali sera za Mugabe wakisema ndizo zilizosababisha uchumi wa nchi hiyo kuanguka vibaya sana.

Post a Comment

 
Top