Mchezaji wa Cameroon Gaelle Enganamouit ameorodheshwa kushindania tuzo ya BBC inayotolewa kwa mchezaji bora wa kike wa mwaka 2016.
Enganamouit, huchezea klabu ya Sweden ya Eskilstuna United, na alikuwa kwenye timu ya Cameroon iliyofika hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la Wanawake mwaka jana.
Cameroon iliondolewa na China.
Wengine wanaopigania tuzo hiyo ni kiungo wa kati wa Ufaransa Amandine Henry, kiungo wa kati wa Scotland Kim Little na wachezaji wa Marekani Carli Lloyd na Becky Sauerbrunn.
Wanaoshindania tuzo:
- Gaelle Enganamouit (Cameroon, fowadi, 23)
- Amandine Henry (Ufaransa, Kiungo wa kati, 26)
- Kim Little (Scotland, Kiungo wa kati, 25)
- Carli Lloyd (Marekani, Kiungo wa kati, 33)
- Becky Sauerbrunn (Marekani, Beki, 30)
Ili kupigia kura mchezaji bora wa kike wa BBC wa mwaka 2016 kupitia SMS, tuma nambari ya mchezaji umpendaye kwa +44 7786 20 20 04.
Tuma 1 kupigia Gaelle Enganamouit, 2 kupigia Amandine Henry, 3 kupigia Kim Little, 4 kupigia Carli Lloyd au 5 kupigia Becky Sauerbrunn.
Ada za kawaida za kutuma ujumbe kimataifa zitatozwa. Tafadhali, thibitisha kwanza na kampuni inayokupa huduma ya simu. Kila namba ya simu inaruhusiwa kupiga kura mara moja pekee.
Mshindi atatangazwa kupitia kituo cha redio cha BBC World Service ana mtandaoni katika bbc.com/womensfootball mnamo Jumanne 24 Mei.
Post a Comment