0
BENKI ya CRDB imesema itatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake watakaotembelea banda lao katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba.
Benki hiyo inashiriki kwenye maonesho hayo ambapo nchi zaidi ya 30 na wafanyabiashara zaidi ya 250 wanashiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei alisema lengo la zawadi hizo ni kuwahamasisha Watanzania kuweka fedha zao benki.
Alisema huduma mbalimbali za kibenki zitafanyika katika banda lao maalumu katika viwanja hivyo, kwani litakuwepo tawi la benki linalohama.
Alisema wateja wa benki hiyo wataweza kupata maelezo ya kampeni inayoendelea ya ‘Shinda na Tembokadi’ ikiwemo kufungua akaunti na kuweka au kutoa fedha zao.

Post a Comment

 
Top