Shirika la kutetea waandishi wa habari, limelalamika juu ya kukamatwa kwa waandishi wa habari wawili wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Kamati ya kulinda waandishi wa habari, CPJ, imesema wanaume hao wawili walikamatwa zaidi ya juma moja lililopita, lakini hawakushtakiwa.
Hapo awali, waliripoti juu ya malalamiko dhidi ya wanajeshi, kwa kuwabughudhi raia, katika mji wa Mahagi, kaskazini mashariki mwa nchi.
CPJ inasema, waandishi wa habari wameonewa mara kadha katika miezi ya karibuni, pamoja na kushambuliwa, kukamatwa kiholela na mitandao kufungwa.
Uchaguzi wa rais unatarajiwa kufanywa mwaka huu katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Post a Comment