Mapigano makali yameripotiwa katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba.
Mapigano hayo yameripotiwa katika maeneo tofauti lakini haijabainika ni nani anayetekeleza mashambulio.
Tayari rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewaagiza raia kuwa watulivu huku ufyatulianaji risasi ukiendelea katika mji huo mkuu, kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Siku ya Alhamisi wanajeshi watano waliuawa na wapiganaji walio watiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.
Kuna serikali ya umoja baada ya kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miaka miwili.
Post a Comment