0
Ripoti iliyosubiriwa sana Uingereza ya uchunguzi kuhusu vita vya Iraq imesema vita hivyo vilianzishwa kabla ya njia zote za kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani kutumiwa.
Akiwasilisha matokeo ya uchunguzi, mwenyekiti wa tume iliyochunguza vita hivyo Sir John Chilcot amesema ni wazi kwamba sera kuhusu Iraq iliongozwa na habari za ujasusi zisizo sahihi na utathmini ambao haukuwa sahihi ambao ulifaa kupingwa.
Vita hivyo vya 2003 viliongozwa na Marekani ikisaidiwa na Uingereza na vilimalizika kwa kuondolewa madarakani kwa Saddam Hussein.
Amesema Iraq haikuwa tishio na uamuzi kuhusu kuwepo kwa silaha za maangamizi makubwa uliwasilishwa kwa ufasaha ambao haukuwa na msingi.
Amesema matokeo ya uvamizi huo ulioongozwa na Marekani yalipuuzwa na kwamba maandalizi ya hali ya baada ya vita hayakufanywa vyema.
BlairImage copyrightGETTY
Image captionBw Blair amesema aliunga mkono vita kwa nia njema
Akijibu ripoti hiyo ya Sir John Chilcot, aliyekuwa waziri mkuu wakati huo Tony Blair amesema: "Siamini kuondolewa madarakani kwa Saddam Hussein ndiko kumesababisha ugaidi tunaoshuhudia sasa Mashariki ya Kati na kwingineko.”
Bw Blair pia amesema uamuzi wake wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Saddam Hussein ilichukuliwa kwa nia njema na kwamba aliamini “ilikuwa kwa maslahi ya taifa”.

Post a Comment

 
Top