0
Mahakama ya Misri imefutilia mbali makubaliano ambayo taifa hilo lingeikabidhi Saudia visiwa viwili vya bahari ya Red Sea.
Uamuzi huo ulipongezwa na wengi katika mahakama hiyo ambao waliimba raia kwenye visiwa hivyo ni Wamisri.
Hatua hiyo ya serikali ya Misri kuvikabidhi visiwa hivyo mnamo mwezi Aprili ilizua hisia kali na kusababisha maandamano mjini Cairo.
Serikali ilidai kwamba Misri iolikuwa ikivisimamia visiwa hivyo ilhali ni vya Saudia.
Rais Abdul Fattah al-Sisi aliidhinisha makubalaino ya kivikabidhi Saudia visiwa hivyo na mchanganuzi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati anasema kuwa uamuzi wa mahakama kwamba hatua hiyo ni kinyume cha sheria itaonekana kuwa aibu kwake.

Post a Comment

 
Top