0
Wizara ya afya nchini imeanzisha kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo kwa watoto dhidi ya maradhi ya ukambi na rubella.
Maafisa wa afya watakuwa wakiwalenga watoto wa umri wa miezi tisa hadi miaka 14.
Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya kuongezeka pakubwa kwa visa vya maambukizi ya maradhi hayo yanayosababisha na virusi, hasa visa vya Rubella.
Maafisa wa afya wanasema karibu Wakenya 400 wamekuwa wakipatikana na virusi vya rubella kila mwaka.
Kwa kawaida, chanjo hiyo hupewa watoto wa umri wa kati ya miezi 9 na 18.

Post a Comment

 
Top