Watu wanafaa kutumia dawa aina ya aspirin mara tu baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi ili kuzuiya athari zaidi zinazosababishwa na ugonjwa huo,watafiti wamesema.
Wanasayansi kutoka chuo cha Oxford wanasema kuwa ijapokuwa madaktari wameagizwa kutoa dawa hiyo kwa wagonjwa,umuhimu wa kuitumia mapema umepuuzwa na matibabu hucheleweshwa.
Wakiandika katika jarida la la afya la Lancet ,wametaka maelezo yalio sahihi kuhusu utumizi wa dawa hiyo.
Ugonjwa wa kiharusi hutokea wakati kuna muingilio wa damu inayoelekea katika ubongo ,na husababisha mikono na miguu kudhoofika mbali na kutatiza mtu anapozungumza huku ishara zake zikipotea katika kipindi cha siku chache.
Lakini uwezekano wa ugonjwa huo kukukabili na nguvu huwa juu siku chache baada ya kumkabili mwathiriwa.
Post a Comment