0
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kuwa uchaguzi wa mwaka ujao hautofanyika ikiwa makimishna wa tume ya uchaguzi hawataondolewa ofisini.
Waziri huyo mkuu wa zamani amekuwa akiongoza maandamano kila Jumatatu katika mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwa makimishna wa tume ya uchaguzi.
Image copyrightAFP
Image captionMaandamano yamekuwa yenye ghasia.
Makimishna hao wamekataa kung'atuka na badala yake kuutaka upinzani kutumia bunge kuwaondoa ofisini.
Baadhi ya maandamano yamekumbwa na ghasia ikiwemo uporaji na ukatili wa polisi ulionaswa na kamera.

Post a Comment

 
Top