Chama tawala cha AK nchini Uturuki kimemchagua Binali Yildirim kama mgombea wa wadhfa wa waziri mkuu baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu kufuatia ugomvi kati yake na rais.
Bwana Yildrim ambaye ndio waziri wa uchukuzi anaonekana kuwa mwandani mkuu wa rais Reccep Tayyip Erdogan.
Waziri mkuu anayeondoka Ahmet Davutoglu alipinga hatua ya rais Erdogan kuimarisha uwezo wake.
Rais huyo alijulikana kutafuta mwandani wake awe waziri mkuu.
Bw Yildirim mwenye umri wa miaka 60 atathibitishwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha AKP katika kikao cha chama kisichokuwa cha kawaida siku ya Jumapili.
Kiongozi wa chama huchukua wadhfa wa waziri mkuu.Ijapokuwa waziri wa kawi nchini humo Berat Albayrak alikuwa ametajwa kuchukua wadhfa huo,jina lake halikuorodheshwa miongoni mwa watu watatu kati ya wabunge na wanachama.
Rais Erdogan ana mipango ya kuifanya Uturuki kufuata mfumo rais mwenye mamlaka badala ya bunge
Post a Comment