0
Watu wenye msimamo wa kadri na wale wanaounga mkono mabadiliko wanakaribia kulidhibiti bunge nchini Iran kufuatia ushindi mkubwa katika uchaguzi ,matokeo ya mapema yameonyesha.
Matokeo ya mapema yanaonyesha wanasiasa wanaomuunga mkono rais Hassan Rouhani wameshinda nusu ya viti 68 vinavyopiganiwa.
Huku wakiungwa mkono na wagombea huru wana uhakika wa ,kuwa wengi bungeni humo.
Image copyrightAP
Image captionrais Rouhani
Raundi ya kwanza ya uchaguzi huo uliwapatia viti 106 kati ya 290 vya bunge hilo.
Katika uchaguzi wa awamu ya pili uliofanyika katika maeneo bunge ambayo wagombea walishindwa kufikisha kiwango cha chini cha asilimia 25 ya kura,wandani wa Rouhani walichukua viti 34 huku wale walio na msimamo mkali wakijipatia viti12.

Post a Comment

 
Top