0
Klabu ya Leicester City imeshinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza. Mwanzo wa msimu Agosti mwaka jana uwezekano wao kushinda ligi ulikuwa umekadiriwa kuwa 5,000/1.
Miezi minane baadaye, ndio mabingwa.
Kwa mujibu wa kampuni ya uwekaji dau ya William Hill, uwezekano wa Leicester kushinda ligi ulikuwa sawa na wa Scott Mills kushinda tuzo ya Oscar. Lakini kuna mambo mengine ya kushangaza zaidi ambao uwezekano wake kutokea ulikuwa juu.
Haya hapa mambo kumi ya kushangaza:

1. Simon Cowell kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza - 500/1

SimonImage copyrightAP
Image captionSimon Cowell na Mwanamfalme Charles
Uwezekano wa Jaji wa kipindi cha televisheni cha X Factor Simon Cowell kuwa waziri mkuu Uingereza ulikuwa mara 10 juu ya uwezekano wa Leicester kushinda taji, katika kampuni ya uwekaji dau ya Ladbrokes.

2. Piers Morgan kuwa meneja wa Arsenal - 2,500/1

Image copyrightGetty Images
Morgan kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi cha Good Morning Britain katika runinga ya ITV. Agosti mwaka jana, uwezekano wake kuingia kwenye soka na kuwa mkufunzi wa Arsenal ulikuwa juu kuliko Leicester kushinda ligi.

3. Sir Alex Ferguson kushinda Strictly Come Dancing - 1,000/1

August 2015, Ladbrokes walikuwa na dau ya meneja wa muda mrefu wa Manchester United Sir Alex Ferguson kushinda Strictly Come Dancing katika 1,000/1.

4. Malkia Elizabeth kuchomoa wimbo wa Krismasi - 1,000/1

Malkia Elizabeth kwa sasa ana umri wa miaka 90, lakini kunao waliodhani angeweza kutoa kibao ambacho kingeongoza katika tasnia ya muziki Krismasi kuliko Leicester kushinda ligi msimu wa 2015/16.

5. Jitu la Loch Ness kupatikana - 500/1

Wengi waliamini picha hii iliashiria uwepo wa jitu kwa jina Loch Ness na mwaka jana Paddy Power walikuwa na dau ya 500/1 ya uwezekano wa jitu hilo kupatikana.
Kulikuwa na habari zaidi mwaka huu kuhusu loch, kwani ilibainika picha hiyo ilitoka kwa mfano wa Loch Ness ulioundwa mwaka 1969 kutumiwa katika filamu ya Sherlock Holmes.

6. Kate na William kujaliwa pacha watatu- 1,000/1

Bintimfalme Charlotte alisherehekea mwaka mmoja tangu kuzaliwa lakini katika Paddy Power dau ya Kate na William kupata pacha watatu ilikuwa na uwezekano wa 1,000/1 Agosti mwaka jana.

7. Dean Gaffney kupata tuzo ya Oscar - 1,000/1

Dean Gaffney alijiondoa kipindi cha EastEnders mwaka 2003, lakini Paddy Power walikuwa na dau ya 1,000/1 ya Gaffney kushinda tuzo ya Oscar ya mwigizaji bora.

8. Kim Kardashian kuwa rais Marekani - 2,000/1

Image copyrightGetty Images
Mumewe, Kanye West, tayari ametangaza atawania urais 2020, lakini kunao walioamini Kim anaweza pia kuwania. Uwezekano wa hilo kutokea katika Paddy Power ulikuwa 2,000/1.

9. Elvis Presley yuko hai? - 2,000/1

Dau ya uwezekano wa mwanamuziki Elvis Presley, aliyefariki 1977, kupatikana akiwa hai na buheri wa afya 2016 ilikuwa na uwezekano wa juu kutokea badala ya Leicester City kushinda Ligi ya Premia.
Paddy Power waliweka nafasi hiyo kuwa 2,000/1.

10. Grimmy kushinda Olimpiki?

Kampuni ya uwekaji dau ya William Hill iliweka uwezekano wa dj wa redioni Radio 1 Nick Grimshaw kushinda dhahabu Michezo ya Olimpiki ya Rio katika kiwango sawa s - 5,000/1 - na Leicester City kushinda ligi ya EPL.

Post a Comment

 
Top