Wasimamizi wa Ligi ya Uhispania wanapanga kuanza kuadhibu klabu ambazo zitaruhusu viti visivyo na mashabiki kuoneshwa kwenye runinga.
Hilo litaanza kutekelezwa kuanzia msimu ujao.
Kanuni mpya zinazitaka klabu za ligi kuu kuhakikisha maeneo yanayoangaziwa na kamera za runinga yamejaa mashabiki.
Lengo la hatua hii ni kuhakikisha viwanja vinavutia zaidi kwa watazamaji na pia kuongeza ushindani wa La Liga dhidi ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Mei 2015, Uhispania ilipitisha sheria mpya za kuwezesha haki za kupeperusha mechi kuunganishwa na kuuzwa pamoja kama fungu moja.
Awali, klabu kama vile Real Madrid na Barcelona zilikuwa zikijitetea kivyake na kupata mikataba ya thamani kubwa
Post a Comment