Je unataka kulipwa mshahara mkubwa ?
Unahitaji kujifunza udaktari au maswala ya kiuchumi.
Utafiti wa mafunzo ya fedha IFS umeripoti kuwa wanafunzi waliosomea utabibu na maswala ya kiuchumi huwa na mshahara mkubwa zaidi baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 10.
Wanaume wanaohitimu katika masomo hayo hujizolea takriban pauni elfu 55,utafiti huo umebaini.
Taaluma zenye faida kubwa | |
---|---|
Shahada | Mapato |
Udaktari | £ 55,000 |
Uchumi | £ 42,000 |
Uhandisi na Teknolojia | £ 31,200 |
Sheria | £ 30,100 |
Sayansi | £ 29,600 |
Elimu | £ 29,600 |
Usanifu mijengo | £ 28,600 |
Hisabati na Sayansi ya Kompyuta | £ 26,800 |
Biashara | £ 26,500 |
Sayansi ya Jamii | £ 26, 200 |
Historia na Falsafa | £ 26,500 |
Bayolojia | £ 25,200 |
Kilimo | £ 21,400 |
Habari na Mawasiliano | £ 19,300 |
Utafiti huu unatilia pondo dhana kuwa shahada za sanaa na ubunifu hazilipi vyema ikilinganishwa na zile za sayansi ama hata sheria.
Mwanafunzi aliyehitimu na shahada ya sanaa na ubunifu anapokea mshahara wa chini wa takriban pauni 14,500.
Vilevile Utafiti huu unasisitiza haja ya kwenda shule.
Mashirika na makampuni yanapendelea wafanyikazi waliohitimu japo na shahada moja kuliko wale ambao hawakufuzu katika vyuo vikuu.Utafiti huu vilevile unathibitisha kuwa wanaume hulipwa zaidi ya wenzao wa kike katika kile sekta ya uchumi.
Bi Anna Vignoles mmoja wa watafiti walioandika ripoti hii wanasema kuwa hii ni fursa kwa manwafunzi yeyote yule achague vyema taaluma anayotaka kujiunga nayo kwani uamuzi wake utakuwa na madhara ya kudumu katika maisha yake ya usoni.
Utafiti huo umegundua kuwa watoto wa matajiri wenyewe pia hupata senti nyingi na kufanikiwa maishani ikilinganishwa na watoto wa masikini.
Hayo yalibainika baada ya utafiti wa kina miongoni mwa wanafunzi 260,000 waliotuma maombi ya ufadhili vyuoni kati ya mwaka wa 2003 hadi mwaka wa 2013.
Post a Comment