0
Timu ya soka ya Leiceister City imeibuka na ushindi baada ya kuifunga 4-0 Swansea city, katika Ligi kuu ya England.
Dakika ya 10 kipindi cha kwanza Riyad Mahrez ameiandikia Leiceister city bao la kuongoza.
Bao la pili limefungwa na mchezaji Leonardo Ulloa dakika ya 30 kipindi cha kwanza,na bao la tatu limefungwa kwa mara nyingine tena na Leonardo Ulloa dakika ya 60 kipindi cha pili.
Marc Albrighton amehitisha ukurasa wa mabao kwa kupachika Bao la Nne na mwisho dakika ya 85 .
katika mchezo wa kwanza wa mapema kabisa Sunderland wakicheza uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Arsenal walitoka bila ya kufungana.

Post a Comment

 
Top