Klabu ya soka ya crystal Palace imetinga hatua ya Fainali ya FA CUP baada ya kuifunga Watford United Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali.
Kwa matokeo hayo ya mchezo huo uliochezwa Uwanjani Wembley, Jijini London, sasa Palace watakutana na Manchester United ambao waliwatoa Everton 2-1 katika Nusu Fainali nyingine.
Hadi Mapumziko Palace walikuwa mbele kwa Bao 1-0 lililofungwa na Yannick Bolasie.
Kipindi cha Pili, Watford walimudu kusawazisha kupitia Deeney lakini Dakika 6 tu baadae Connor Wickham akafunga Bao la Pili na la ushindi kwa Palace.
Fainali Michuano hii itachezwa Mei 21 hapo hapo katika dimba laaWembley
Post a Comment