0
Klabu ya soka ya Azam fc imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA CUP) baada ya kuibwaga Mwadui FC kwa Penati 5-3
Klabu ya soka ya Azam fc imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA CUP) baada ya kuibwaga Mwadui FC kwa Penati 5-3
Penalti hizo zilipigwa baada ya Sare ya 2-2 katika Dakika 120 za Mchezo.
Azam FC walitangulia kuifunga Mwadui FC kwa Bao la Dakika ya 3 la Mcha na Mwadui FC kusawazisha Dakika ya 82 kupitia Kabunda.
Mechi ikaenda Dakika za Nyongeza 30 na kila Timu kufunga Bao 1 zaidi kwa Mcha kuipa Azam Bao la Pili Dakika ya 97 na Mwadui kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 123 kwa Bao la Aziz.
Mechi kati ya Coastal Union na Yanga imevunjika baada ya kuchezwa Dakika 15 tu za Dakika za Nyongeza 30 huku Yanga wakiongoza 2-1.
Huko Mkwakwani Tanga Coastal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 55 la Yusu Sabo na Donald Ngoma kuisawazishia Yanga katika Dakika ya 61.
Bao hizo zilibaki hadi Dakika 90 zinakwisha na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30 na yanga kufanikiwa kuandika Bao lao la Pili Dakika ya 95 Mfungaji akiwa Amisi Tambwe.
Dakika ya 101, Coastal walibaki Mtu 10 baada ya Adeyum Ahmed kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hadi Dakika 15 za kwanza kumalizika, Yanga walikuwa mbele kwa Bao 2-1 lakini Mechi hii ikavunjika kutokana na vurugu za Mashabiki huku pia giza likishamiri Uwanjani.
Hivyo ripoti ya kutoka kwa kamisaa wa mchezo pamoja na kamati ya mashindano itatoa majibu sahii kuhusiana na mchezo huo.pigwa baada ya Sare ya 2-2 katika Dakika 120 za Mchezo.

Post a Comment

 
Top