0
Israeli imeondoa mitambo ya kutambua chuma iliyosababisha utata mkubwa, ambayo ilikuwa imewekwa katika eneo takatifu mjini Jerusalem, ambalo waislamu wanapaita Haram al-Sharif na kwa wayahudi Hekalu la mlimani.
Maafisa wakuu sasa wanasema kuwa, mitambo mingine ya uchunguzi, itawekwa ambayo haitatizi pakubwa waumini wanaofika kwa maombi.
Ghasia zilizuka wakati polisi wawili wa Israel waliuawa tarehe 14 mwezi huu.
Israel ilisema kuwa mitambo hiyo ilihitajika kwa sababu watu walikuwa wakiingia na silaha katika eneo hilo takatifu.
Lakini hatua hiyo ilichochea maandamano.
Ijumaa iliyopita wapalestina watatu waliuawa kwenye ghasia na vikosi vya usalama vya Israel, wakati maefu ya waandamanaji walifika eneo la Jerusalem mashariki na ukingo wa magharibi linalokaliwa na Israel.
Israel pia inasema kuwa wafanyikazi wake wote waliokuwa wakifanya kazi katika ubalozi wake ulioko Jordan, wamewasili nyumbani, akiwemo mlinzi wa usalama ambaye alihusika katika kisa cha hapo jana Jumatatu, cha ufyatulianaji wa risasi, ambapo raia wawili wa Jordan waliuwawa

Post a Comment

 
Top