Kundi la Islamic State limethibitisha kifo cha mmoja wa Makamanda wake wa ngazi za juu kijeshi, Omar Shishani.
Shirika la Habari la Amaq limesema Shishani, AMBAYE Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilimuelezea kama ''Waziri wa Ulinzi'' wa kundi hilo la wapiganaji, ameuawa katika mji wa Shirqatkusini ya Mosul nchini Iraq.
Shishani, akijulikana pia kama Omar Chechen, aliwahi kuripotiwa kuwa amekufa zaidi ya mara moja.
Mwezi Machi maafisa wa jeshi la Marekani walisema kwamba ameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na nchi hiyo, Syria.
Kamanda huyo wa ngazi za juu alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Is,wanaosakwa sana na Marekani, ambapo kilitolewa kiasi cha dola milioni tano kwa mtu atakayemkamata.
Post a Comment